WILFRIED ZAHA hakuweza kukataa uhamisho wa £15million kwenda Manchester United — japokuwa ni mshabiki wa damu wa klabu ya Arsenal.
Winga huyo ambaye anachezea Crystal Palace kwa mkopo, ni mshabiki wa tangu utotoni wa Gunners, na alikuwa na ndoto na kujiunga na Arsenal kabla ya United hawajaingia katika mbio za kumsaini.
Zaha, 20, alisajiliwa na United mwezi January kabla ya kurudishwa Palace kwa mkopo.
Winga huyo alisema: “Siku zote ilikuwa ni Arsenal, Arsenal, Arsenal, Arsenal katika kuchagua timu ambayo ningejiunga nayo.
“Siku zote nimekuwa mshabiki wa Arsenal. Sikudhani kama United watakuja kunihitaji lakini ikawa vinginevyo. Arsenal ni timu nzuri lakini United ni moja ya klabu kubwa sana duniani ilinibidi nijiunge nayo.
Comments
Post a Comment