Kikosi
cha timu ya Young Africans leo kimeendelea na mazoezi asubuhi katika
uwanja wa mabatini Kijitonyama kujiandaa na mchezo wa mzunguko wa pili
wa Ligi ya Vodacom dhidi ya timu ya Toto African siku ya jumamosi Machi
09 ,2013 katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Young
Africans ambayo inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa kuwa na
pointi 42 na mabao 35 ya kufunga na mabao 12 ya kufunga, iko mbele kwa
pointi sita zaidi ya timu ya Azam inayoshika nafasi ya pili kwa kuwa na
ponti 36 na mabao 31 ya kufunga na mabao 15 ya kufungwa.
Mara
baada ya kupata ushindi wa tatu mfululizo katika michezo ya Ligi Kuu ya
Vodacom, kikosi cha mholanzi Ernest Brandts kiliendelea na mazoezi
katika Uwanja wa mabatini Kijitonyama siku ya alhamis na ijumaa kabla ya
kupewa mapumziko ya siku mbili jumamosi na jumapili.
Katika
mchezo wa mwisho Young Africans iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya
timu ya Kagera Sugar bao lililofungwa na kiungo Haruna Niyonzima, tangu
mzunguko wa pili uanze Yanga imeshacheza jumla ya michezo mitano na
kufanikiwa kushinda michezo minne na kutoka sare mmoja hivyo
kujikusanyia point 13 kati ya 15.
Ili
kujiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa Ubingwa, Kocha Mkuu Brandts
amesema anakianadaa kikosi chake kuhakikisha kinapata pointi 3 katika
kila mchezo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa Ubingwa.
Kila
mchezo tunaocheza kwa sasa ni fainali kwetu, kila timu inahitaji kupata
pointi ili kujiweka katika nafasi nzuri, na sisi pia tunahitaji kupata
pointi 3 katika kila mchezo hali inayopelekea mechi kuwa ngumu, lakini
kikubwa nimekiandaa kikosi changu kuhakikisha kinaibuka na pointi 3
katika kila mchezo alisema 'Brandts'.
Comments
Post a Comment