Haukuwa
mchezo mchezo ambao Barcelona walionyesha kiwango kikubwa, lakini Xavi
alikuwa na usiku mzuri kuliko: akipiga pasi 96 na zote zikiwa
zimewafikia walengwa - kwa maana hakupoteza pasi katika mchezo wa robo
fainali dhidi ya Paris St Germain.
Wakatalunya
walikuwa kwenye hatari ya kukosa kucheza nusu fainali ya Champions
League kwa mara ya 6 mfululizo baada ya kuwa nyuma baada ya dakika 50 ya
mchezo huo, lakini wakaweza kurudisha goli dakika ya 71 likifungwa na
Pedro.
Wengi watazungumzia kuhusu mabadiliko ya timu baada ya Messi kuingia, lakini ilikuwa ni Xavi aliyekuwa kwenye kiwango akikiongoza kiungo cha Barca kupeleka mashambulizi mbele aliyeleta utofauti mkubwa.
Mhispania huyo
mwenye miaka 33, alicheza dakika 90 na kufanikiwa kutopoteza pasi hate
moja - na kuweka rekodi mpya ambayo haijawahi kufikiwa na mchezaji
yoyote.
Xavi aliweza
kuipita rekodi ya Javier Zanetti dhidi ya Tottenham aliyoiweka miaka
mitatu iliyopita, Emmanuel Eboue anashika nafasi ya taut kwenye list ya
wachezaji waliopiga pasi nyingi kwenye mchezo mmoja.
Wakati mhispania akikaribia kutimiza pasi 100, Zanetti na Eboue walipiga pasi 72 na 54 katika me chi zao walizocheza.
Comments
Post a Comment