MOYES AANZA KAZI RASMI

Kocha huyo wa zamani wa Everton leo asubuhi ndio ameanza rasmi kazi ya kuwa boss wa benchi la ufundi la Manchester United akirithi mikoba ya msoctland mwenzie Alex Ferguson.
Moyes aliwasili katika kituo cha mazoezi cha Carrington mnamo saa mbili asubuhi akiendesha gari la alilopewa na wadhamini wa klabu hiyo Chevrolet. 

Aliwapungia mkono waandishi wa habari huku akitabasamu nje ya uwanja wa Carrington kabla ya kuingia ndani na kuanza rasmi kazi yake ya kupeleka mbele gurudumu la United.

Wakati huo huo Manchester United leo imethibitisha uteuzi wa makocha Steve Round atakayekuwa msaidizi wa Moyes,  Chris Woods kocha wa makipa na Jimmy Lumsden


Comments